Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Sam 15

15
Sauli Awashinda Waamaleki lakini Amsalimisha Mfalme wao
1 # 1 Sam 10:1; 9:16 Wakati huo Samweli akamwambia Sauli, BWANA alinipeleka nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na maneno ya BWANA. 2#Kut 17:8-14; Kum 25:17-19BWANA wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. 3#Law 27:28; Yos 6:17; Kut 20:5; Isa 14:21; Mwa 3:17; Yos 7:24Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng’ombe na kondoo, ngamia na punda. 4#Yos 15:24Ndipo Sauli akawaita watu, akawahesabu huko Telemu, askari waliopanda farasi mia mbili elfu, na watu wa Yuda kumi elfu. 5Sauli akaufikilia mji wa Amaleki, akauvizia bondeni. 6#Hes 24:21; Amu 1:16; 4:11; Mwa 18:25; 19:12; Mdo 2:40; Ufu 18:4; Kut 18:10; Hes 10:29Sauli akawaambia Wakeni, Haya! Enendeni zenu, mkashuke ili kujitenga na Waamaleki, nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao; maana mliwatendea wana wa Israeli mema, walipopanda kutoka Misri. Basi hao Wakeni wakaondoka, wakajitenga na Waamaleki. 7#1 Sam 14:48; Mwa 2:11; 25:18; 16:7; 1 Sam 27:8Sauli akawapiga Waamaleki, toka Havila uendapo Shuri, unaokabili Misri. 8#1 Fal 20:34; Est 3:1; 1 Sam 30:1Akamkamata Agagi, mfalme wa Waamaleki, yu hai, akawaangamiza hao watu wote kwa upanga. 9#Mit 15:27; 1 Tim 6:10Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng’ombe, na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa.
Sauli Akataliwa kama Mfalme
10Ndipo neno la BWANA likamjia Samweli, kusema, 11#Mwa 6:6; 2 Sam 24:16; Yos 22:16; 1 Fal 9:6; Zab 36:3; Sef 1:6; Mt 24:13; 1 Sam 16:1; Lk 19:41,44; Rum 9:1-3Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia BWANA usiku kucha. 12#Yos 15:55Samweli akaondoka asubuhi na mapema ili aonane na Sauli; Samweli akaambiwa ya kwamba, Sauli alifika Karmeli, na tazama, akajisimamishia ukumbusho, akageuka, akapita, akatelemkia Gilgali. 13#Mwa 14:19; Amu 17:2; Rut 3:2; Lk 18:11Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na BWANA, nimeitimiza amri ya BWANA. 14Samweli akasema, Maana yake nini, basi, hiki kilio cha kondoo masikioni mwangu, na huu mlio wa ng’ombe ninaousikia? 15#Mwa 3:12; Mit 28:13Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng’ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa. 16Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami nitakuambia neno aliloniambia BWANA usiku huu. Naye akamwambia, Haya, sema. 17Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha kabila za Israeli? Naye BWANA akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli. 18Kisha BWANA akakutuma safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hata watakapoangamia. 19Mbona, basi, hukuitii sauti ya BWANA, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA? 20Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya BWANA, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa. 21Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng’ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, huko Gilgali.
22 # Zab 50:8,9; Mit 21:3; Isa 1:11; Yer 7:22; Amo 5:21,24; Mik 6:6; Mt 9:13; 12:7; Ebr 10:6; Kut 19:5; Mhu 5:1; Yer 7:23; Hos 6:6; Mt 5:24; 9:13; Mk 12:33 Naye Samweli akasema,
je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu
Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA?
Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu,
Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.
23 # Kum 18:10 Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi,
Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago;
Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA,
Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.
24 # 2 Sam 12:13; Kut 9:27; Mt 27:4; Kut 23:2; Ayu 31:34; Mit 29:25; Isa 51:12; Lk 23:20-25; Ufu 21:8 Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeihalifu amri ya BWANA, pia na maneno yako; kwa sababu naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao. 25Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja nami, nipate kumwabudu BWANA. 26#1 Sam 2:30Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli. 27#1 Sam 28:17; 1 Fal 11:30-31Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka. 28Basi Samweli akamwambia, Leo BWANA amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe. 29#Hes 23:19; Eze 24:14; 2 Tim 2:13; Tit 1:2Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute. 30#1 Sam 2:30; Zab 49:20; Mit 4:8; 26:1; Yn 5:44; 12:43; Rum 2:28,29Akasema, Nimekosa; lakini uniheshimu sasa, nakuomba, mbele ya wazee wa watu wangu, na mbele ya Israeli, rudi pamoja nami, nimwabudu BWANA, Mungu wako. 31Basi Samweli akarudi na kuandamana na Sauli; naye Sauli akamwabudu BWANA.
32Ndipo Samweli akasema, Nileteeni hapa Agagi, mfalme wa Waamaleki. Basi Agagi akamwendea kwa utepetevu. Naye Agagi akasema, Bila shaka uchungu wa mauti umeondoka. 33#Mwa 9:6; Kut 17:11; Amu 1:7; Mt 7:2; Yak 2:13; Ufu 16:6; 18:6; 1 Fal 18:40Lakini Samweli akamjibu, Kama upanga wako ulivyofanya wanawake kufiwa na watoto wao, vivyo hivyo mama yako atafiwa miongoni mwa wanawake. Basi Samweli akamkata Agagi vipande mbele za BWANA huko Gilgali.
34 # 1 Sam 11:4 Na baada ya hayo Samweli akaenda zake kule Rama; naye Sauli akakwea kwenda nyumbani kwake huko Gibea ya Sauli. 35Wala Samweli hakuenda tena kuonana na Sauli hata siku ya kufa kwake; lakini Samweli alikuwa akimlilia Sauli; naye BWANA akaghairi ya kuwa amemtawaza Sauli awe mfalme juu ya Israeli.

Iliyochaguliwa sasa

1 Sam 15: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha