Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Samweli 15

15
Sauli awashinda Waamaleki lakini amsalimisha mfalme wao
1 # 1 Sam 10:1; 9:16 Samweli akamwambia Sauli, BWANA alinituma nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na maneno ya BWANA. 2#Kut 17:8-14; Kum 25:17-19 BWANA wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu yale ambayo Waamaleki waliwatenda Waisraeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. 3#Law 27:28; Yos 6:17; Kut 20:5; Isa 14:21; Mwa 3:17; Yos 7:24 Basi sasa nenda ukawapige Waamaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, na mtoto anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda. 4#Yos 15:24 Ndipo Sauli akawaita watu, akawahesabu huko Telemu, askari wa miguu elfu mia mbili na watu elfu kumi wa Yuda. 5Sauli akaufikia mji wa Amaleki, akauvizia bondeni. 6#Hes 24:21; Amu 1:16; 4:11; Mwa 18:25; 19:12; Mdo 2:40; Ufu 18:4; Kut 18:10; Hes 10:29 Sauli akawaambia Wakeni, Haya! Nendeni zenu, mkashuke ili kujitenga na Waamaleki, nisije nikawaangamiza ninyi pamoja nao; maana mliwatendea wana wa Israeli mema, walipopanda kutoka Misri. Basi hao Wakeni wakaondoka, wakajitenga na Waamaleki. 7#1 Sam 14:48; Mwa 2:11; 25:18; 16:7; 1 Sam 27:8 Sauli akawapiga Waamaleki, toka Havila hadi Shuri, mashariki mwa Misri. 8#1 Fal 20:34; Est 3:1; 1 Sam 30:1 Akamkamata Agagi, mfalme wa Waamaleki akiwa hai, akawaangamiza hao watu wote kwa upanga. 9#Mit 15:27; 1 Tim 6:10 Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na chochote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali chochote kilichokuwa kibaya na kisichofaa, ndicho walichoangamiza kabisa.
Sauli akataliwa kama mfalme
10Ndipo neno la BWANA likamjia Samweli, kusema, 11#Mwa 6:6; 2 Sam 24:16; Yos 22:16; 1 Fal 9:6; Zab 36:3; Sef 1:6; Mt 24:13; 1 Sam 16:1; Lk 19:41,44; Rum 9:1-3 Najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli akasikitika, akamlilia BWANA usiku kucha. 12#Yos 15:55 Samweli akaondoka asubuhi na mapema ili aonane na Sauli; Samweli akaambiwa ya kwamba, Sauli alifika Karmeli, na tazama, akajisimamishia mnara wa ukumbusho wake, akageuka, akapita, akateremkia Gilgali. 13#Mwa 14:19; Amu 17:2; Rut 3:2; Lk 18:11 Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na BWANA, nimeitimiza amri ya BWANA. 14Samweli akasema, Maana yake nini basi, hiki kilio cha kondoo masikioni mwangu, na huu mlio wa ng'ombe ninaousikia? 15#Mwa 3:12; Mit 28:13 Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng'ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa. 16Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami nitakuambia neno aliloniambia BWANA usiku huu. Naye akamwambia, Haya, sema. 17Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha makabila ya Israeli? Naye BWANA akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli. 18Kisha BWANA akakutuma safarini, akasema, Nenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hadi watakapoangamia. 19Mbona basi hukuitii sauti ya BWANA, bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA? 20Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya BWANA, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa. 21Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng'ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, huko Gilgali.
22 # Zab 50:8,9; Mit 21:3; Isa 1:11; Yer 7:22; Amo 5:21,24; Mik 6:6; Mt 9:13; 12:7; Ebr 10:6; Kut 19:5; Mhu 5:1; Yer 7:23; Hos 6:6; Mt 5:24; 9:13; Mk 12:33 Naye Samweli akasema,
Je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu
Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA?
Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu,
Na kusikiza ushauri kuliko mafuta ya beberu.
23 # Kum 18:10 Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi,
Na ukaidi ni kama uovu na kuabudu vinyago;
Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA,
Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.
24 # 2 Sam 12:13; Kut 9:27; Mt 27:4; Kut 23:2; Ayu 31:34; Mit 29:25; Isa 51:12; Lk 23:20-25; Ufu 21:8 Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeivunja amri ya BWANA, pia na maneno yako; kwa sababu niliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao. 25Basi sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja nami, nipate kumwabudu BWANA. 26#1 Sam 2:30 Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli. 27#1 Sam 28:17; 1 Fal 11:30-31 Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka. 28Basi Samweli akamwambia, Leo BWANA amekurarulia ufalme wa Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko wewe. 29#Hes 23:19; Eze 24:14; 2 Tim 2:13; Tit 1:2 Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute. 30#1 Sam 2:30; Zab 49:20; Mit 4:8; 26:1; Yn 5:44; 12:43; Rum 2:28,29 Akasema, Nimekosa; lakini uniheshimu sasa, nakuomba, mbele ya wazee wa watu wangu, na mbele ya Israeli, rudi pamoja nami, nimwabudu BWANA, Mungu wako. 31Basi Samweli akarudi na kuandamana na Sauli; naye Sauli akamwabudu BWANA.
32Ndipo Samweli akasema, Nileteeni hapa Agagi, mfalme wa Waamaleki. Basi Agagi akamwendea kwa ulegevu.#15:32 maana katika Kiebrania si dhahiri. Naye Agagi akasema, Bila shaka uchungu wa mauti umeondoka. 33#Mwa 9:6; Kut 17:11; Amu 1:7; Mt 7:2; Yak 2:13; Ufu 16:6; 18:6; 1 Fal 18:40 Lakini Samweli akamjibu, Kama upanga wako ulivyofanya wanawake kufiwa na watoto wao, vivyo hivyo mama yako atafiwa miongoni mwa wanawake. Basi Samweli akamkata Agagi vipande mbele za BWANA huko Gilgali.
34 # 1 Sam 11:4 Na baada ya hayo Samweli akaenda zake kule Rama; naye Sauli akakwea kwenda nyumbani kwake huko Gibea ya Sauli. 35Wala Samweli hakuenda tena kuonana na Sauli hata siku ya kufa kwake; lakini Samweli alikuwa akimlilia Sauli; naye BWANA akaghairi ya kuwa amemtawaza Sauli awe mfalme juu ya Israeli.

Iliyochaguliwa sasa

1 Samweli 15: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha