Methali 29:2-4
Methali 29:2-4 BHN
Waadilifu wakitawala watu hufurahi, lakini waovu wakitawala watu hulalamika. Apendaye hekima humfurahisha baba yake; lakini aandamanaye na malaya hufuja mali yake. Mfalme akitumia haki huipatia nchi uthabiti, lakini akipenda hongo taifa huangamia.