Methali 29:2-4
Methali 29:2-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Waadilifu wakitawala watu hufurahi, lakini waovu wakitawala watu hulalamika. Apendaye hekima humfurahisha baba yake; lakini aandamanaye na malaya hufuja mali yake. Mfalme akitumia haki huipatia nchi uthabiti, lakini akipenda hongo taifa huangamia.
Methali 29:2-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua. Apendaye hekima humfurahisha babaye; Bali ashikamanaye na makahaba hutapanya mali. Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.
Methali 29:2-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi; Bali mwovu atawalapo, watu huugua. Apendaye hekima humfurahisha babaye; Bali ashikamanaye na makahaba hutapanya mali. Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.
Methali 29:2-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi; waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni. Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake. Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti, bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza.