Methali 28:8-10
Methali 28:8-10 BHN
Aongezaye mali yake kwa riba na kutoza faida anamkusanyia mwingine mwenye kuwahurumia maskini. Anayekataa kuisikia sheria, huyo hata sala yake ni chukizo kwa Mungu. Anayemshawishi mtu mwema kutenda mabaya, ataanguka katika shimo lake mwenyewe. Wasio na hatia wamewekewa mema yao.