Methali 28:8-10
Methali 28:8-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Aongezaye mali yake kwa riba na kutoza faida anamkusanyia mwingine mwenye kuwahurumia maskini. Anayekataa kuisikia sheria, huyo hata sala yake ni chukizo kwa Mungu. Anayemshawishi mtu mwema kutenda mabaya, ataanguka katika shimo lake mwenyewe. Wasio na hatia wamewekewa mema yao.
Methali 28:8-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini. Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo. Kila mtu awapotezaye wenye haki katika njia mbaya, Ataanguka katika rima lake mwenyewe; Bali wakamilifu watarithi mema.
Methali 28:8-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini. Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo. Kila mtu awapotezaye wenye haki katika njia mbaya, Ataanguka katika rima lake mwenyewe; Bali wakamilifu watarithi mema.
Methali 28:8-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Yeye aongezaye utajiri wake kwa riba kubwa mno hukusanya kwa ajili ya mwingine, ambaye atawahurumia maskini. Mtu yeyote akikataa kusikia sheria, hata maombi yake ni chukizo. Yeye anayemwongoza mwenye haki kwenye mapito mabaya, ataanguka kwenye mtego wake mwenyewe, bali wasio na lawama watapokea urithi mwema.