Methali 27:4-6
Methali 27:4-6 BHN
Ghadhabu ni katili na hasira huangamiza; lakini ni nani awezaye kuukabili wivu? Afadhali mtu anayekuonya waziwazi, kuliko yule afichaye upendo. Makaripio ya rafiki yaonesha uaminifu, lakini busu la adui ni udanganyifu.