Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 26:13-22

Methali 26:13-22 BHN

Mvivu husema: “Huko nje kuna simba; siwezi kwenda huko.” Kama vile mlango uzungukiapo bawaba zake, ndivyo mvivu juu ya kitanda chake. Mvivu huutia mkono wake katika sahani ya chakula, lakini hawezi kuuinua hadi mdomoni. Mvivu hujiona kuwa mwenye hekima kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara. Ajiingizaye katika ugomvi usiomhusu, ni kama mtu amshikaye masikio mbwa anayepita. Kama mwendawazimu achezeavyo mienge, au mishale ya kifo, ndivyo alivyo mtu ampotoshaye jirani, kisha aseme, “Nilikuwa natania tu!” Bila kuni, moto huzimika; bila mchochezi, ugomvi humalizika. Kama vile makaa au kuni huchochea moto, ndivyo mgomvi achocheavyo ugomvi. Maneno ya msengenyaji ni kama kitoweo; hushuka mpaka ndani kabisa tumboni.

Soma Methali 26