Methali 26:13-22
Methali 26:13-22 Biblia Habari Njema (BHN)
Mvivu husema: “Huko nje kuna simba; siwezi kwenda huko.” Kama vile mlango uzungukiapo bawaba zake, ndivyo mvivu juu ya kitanda chake. Mvivu huutia mkono wake katika sahani ya chakula, lakini hawezi kuuinua hadi mdomoni. Mvivu hujiona kuwa mwenye hekima kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara. Ajiingizaye katika ugomvi usiomhusu, ni kama mtu amshikaye masikio mbwa anayepita. Kama mwendawazimu achezeavyo mienge, au mishale ya kifo, ndivyo alivyo mtu ampotoshaye jirani, kisha aseme, “Nilikuwa natania tu!” Bila kuni, moto huzimika; bila mchochezi, ugomvi humalizika. Kama vile makaa au kuni huchochea moto, ndivyo mgomvi achocheavyo ugomvi. Maneno ya msengenyaji ni kama kitoweo; hushuka mpaka ndani kabisa tumboni.
Methali 26:13-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani, Simba yuko katika njia kuu. Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake; Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake. Mtu mvivu hutia mkono wake katika sahani; Kwamchosha kuupeleka tena kinywani pake. Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake, Kuliko watu saba wawezao kutoa sababu. Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake; Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake. Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge, Na mishale, na mauti; Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake, Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu? Moto hufa kwa kukosa kuni; Na bila mchongezi fitina hukoma. Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, Na kama kuni juu ya moto; Ndivyo mtu mgomvi achocheavyo uadui. Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo. Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.
Methali 26:13-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani, Simba yuko katika njia kuu. Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake; Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake. Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini; Kwamchosha kuupeleka tena kinywani pake. Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake, Kuliko watu saba wawezao kutoa sababu. Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake; Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake. Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge, Na mishale, na mauti; Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake, Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu? Moto hufa kwa kukosa kuni; Na bila mchongezi fitina hukoma. Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, Na kama kuni juu ya moto; Ndivyo mtu mgomvi achocheavyo uadui. Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo. Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.
Methali 26:13-22 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mvivu husema, “Yuko simba barabarani, simba mkali anazunguka mitaa!” Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake, ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake. Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, naye huchoka kuupeleka kwenye kinywa chake. Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe, kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara. Kama yeye amkamataye mbwa kwa masikio, ndivyo alivyo mtu apitaye njiani na kujiingiza kwenye ugomvi usiomhusu. Kama mwendawazimu atupaye mishale ya moto ya kufisha, ndivyo alivyo mtu amdanganyaye jirani yake na kusema, “Nilikuwa nikifanya mzaha tu!” Bila kuni moto huzimika; pasipo uchongezi ugomvi humalizika. Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, na kama kuni kwenye moto, ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuchochea ugomvi. Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu; huingia sehemu za ndani sana za mtu.