Methali 24:15-18
Methali 24:15-18 BHN
Usivizie kama mwovu kushambulia makao ya mtu mwema, wala usijaribu kuiharibu nyumba yake, maana mtu mwema huanguka mara nyingi lakini huinuka, lakini mtu mwovu huangamizwa na janga. Usishangilie kuanguka kwa adui yako; usifurahie moyoni mwako kujikwaa kwake, maana Mwenyezi-Mungu aonaye hayo hatapendezwa; huenda akaacha kumwadhibu.