Mithali 24:15-18
Mithali 24:15-18 NENO
Usivizie kama haramia afanyavyo ili kuyashambulia makao ya mwenye haki, wala usiyavamie makazi yake, kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena; lakini waovu huangushwa chini na maafa. Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo; wakati anapojikwaa, usiruhusu moyo wako ushangilie. BWANA asije akaona na kuchukia akaiondoa ghadhabu yake mbali naye.