Methali 23:19-22
Methali 23:19-22 BHN
Sikia mwanangu, uwe na hekima; fikiria sana jinsi unavyoishi. Usiwe mmoja wa walevi wa divai, wala walafi wenye kupenda nyama, maana walevi na walafi wataishia kuwa maskini, anayetumia siku yake kusinzia atavaa matambara. Msikilize baba yako aliyekuzaa, wala usimdharau mama yako akizeeka.