Mithali 23:19-22
Mithali 23:19-22 NENO
Sikiliza, mwanangu na uwe na hekima, weka moyo wako kwenye njia iliyo sawa. Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo, au wale walao nyama kwa pupa, kwa maana walevi na walafi huwa maskini, nako kusinzia huwavika matambara. Msikilize baba yako, aliyekuzaa, wala usimdharau mama yako atakapokuwa mzee.