Methali 21:14-16
Methali 21:14-16 BHN
Hasira hutulizwa kwa zawadi ya siri; tunu apewayo mtu imefichwa hupooza ghadhabu. Haki ikitekelezwa watu wema hufurahi, lakini watu waovu hufadhaishwa. Anayetangatanga mbali na njia ya busara, atajikuta ametua miongoni mwa wafu.