Mithali 21:14-16
Mithali 21:14-16 NENO
Zawadi inayotolewa kwa siri hutuliza hasira, na rushwa iliyofichwa kwenye nguo hutuliza ghadhabu kali. Wakati haki imetendeka, huleta furaha kwa wenye haki, bali hofu kwa watenda maovu. Mtu anayepotea kutoka mapito ya ufahamu, hupumzika katika kundi la waliokufa.