Methali 21:14-16
Methali 21:14-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Hasira hutulizwa kwa zawadi ya siri; tunu apewayo mtu imefichwa hupooza ghadhabu. Haki ikitekelezwa watu wema hufurahi, lakini watu waovu hufadhaishwa. Anayetangatanga mbali na njia ya busara, atajikuta ametua miongoni mwa wafu.
Methali 21:14-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kipawa cha siri hutuliza hasira; Na rushwa bindoni humliza ghadhabu kali. Ni furaha yao wenye haki kutenda hukumu; Lakini ni uharibifu kwao watendao maovu. Mtu aikosaye njia ya busara Atakaa katika mkutano wao waliokufa.
Methali 21:14-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kipawa cha siri hutuliza hasira; Na rushwa bindoni humliza ghadhabu kali. Ni furaha yao wenye haki kutenda hukumu; Lakini ni uharibifu kwao watendao maovu. Mtu aikosaye njia ya busara Atakaa katika mkutano wao waliokufa.
Methali 21:14-16 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Zawadi inayotolewa kwa siri hutuliza hasira, na rushwa iliyofichwa kwenye nguo hutuliza ghadhabu kali. Wakati haki imetendeka, huleta furaha kwa wenye haki, bali hofu kwa watenda maovu. Mtu anayepotea kutoka mapito ya ufahamu, hupumzika katika kundi la waliokufa.