Methali 15:1-3
Methali 15:1-3 BHN
Kujibu kwa upole hutuliza hasira, lakini neno kali huchochea hasira. Ulimi wa mwenye hekima hueneza maarifa, lakini watu wapumbavu hububujika upuuzi. Macho ya Mwenyezi-Mungu huona kila kitu, humchunguza mtu mwema na mtu mbaya.