Mit 15:1-3
Mit 15:1-3 SUV
Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu. Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu. Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.