Methali 15:1-3
Methali 15:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Kujibu kwa upole hutuliza hasira, lakini neno kali huchochea hasira. Ulimi wa mwenye hekima hueneza maarifa, lakini watu wapumbavu hububujika upuuzi. Macho ya Mwenyezi-Mungu huona kila kitu, humchunguza mtu mwema na mtu mbaya.
Shirikisha
Soma Methali 15Methali 15:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu. Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu. Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.
Shirikisha
Soma Methali 15Methali 15:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu. Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu. Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.
Shirikisha
Soma Methali 15