Zaburi 105:12-15
Zaburi 105:12-15 SRUV
Walipokuwa watu wawezao kuhesabiwa, Naam, watu wachache na wageni katika nchi, Wakatangatanga toka taifa hadi taifa, Toka ufalme mmoja hadi kwa watu wengine. Hakumwacha mtu awaonee, Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao. Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.

