Zaburi 105:12-15
Zaburi 105:12-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Watu wa Mungu walikuwa wachache; hawakuwa maarufu, tena walikuwa wageni nchini Kanaani. Walitangatanga kutoka taifa hadi taifa; kutoka nchi moja hadi nchi nyingine. Lakini Mungu hakuruhusu mtu awadhulumu; kwa ajili yao aliwaonya wafalme: “Msiwaguse wateule wangu; msiwadhuru manabii wangu!”
Zaburi 105:12-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Walipokuwa watu wawezao kuhesabiwa, Naam, watu wachache na wageni katika nchi, Wakatangatanga toka taifa hadi taifa, Toka ufalme mmoja hadi kwa watu wengine. Hakumwacha mtu awaonee, Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao. Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.
Zaburi 105:12-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Walipokuwa watu wawezao kuhesabiwa, Naam, watu wachache na wageni ndani yake, Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa, Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine. Hakumwacha mtu awaonee, Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao. Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.
Zaburi 105:12-15 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Walipokuwa wachache kwa idadi, wachache sana na wageni ndani yake, walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine. Hakuruhusu mtu yeyote awadhulumu; kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema: “Msiwaguse niliowapaka mafuta; msiwadhuru manabii wangu.”