Mithali 28:8-10
Mithali 28:8-10 SRUV
Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini. Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo. Kila mtu awapotezaye wenye haki katika njia mbaya, Ataanguka katika rima lake mwenyewe; Bali wakamilifu watarithi mema.