Mithali 23:19-22
Mithali 23:19-22 SRUV
Sikia, mwanangu, uwe na hekima, Na kuuongoza moyo wako katika njia njema. Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa. Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu. Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.