1 Mambo ya Nyakati 4:1-8
1 Mambo ya Nyakati 4:1-8 SRUV
Wana wa Yuda; Peresi, na Hesroni, na Karmi, na Huri, na Shobali. Na Reaya, mwana wa Shobali, akamzaa Yahathi; na Yahathi akawazaa Ahumai, na Lahadi. Hizo ndizo jamaa za Wasorathi. Na hawa ndio wana wa babaye Etamu; Yezreeli, na Ishma, na Idbashi; na dada yao aliitwa jina lake Haselelponi; na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, babaye Bethlehemu. Naye Ashuri, babaye Tekoa, alikuwa na wake wawili, Hela na Naara. Naye Naara akamzalia Ahuzamu, na Heferi, na Temeni, na Ahashtari. Hao ndio wana wa Naara. Na wana wa Hela walikuwa Serethi, na Ishari, na Ethnani. Na Hakosi akawazaa Anubu, na Sobeba, na jamaa za Aharheli, mwana wa Harumu.