Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nyakati 4:1-8

1 Nyakati 4:1-8 NENO

Wazao wa Yuda walikuwa: Peresi, Hesroni, Karmi, Huri na Shobali. Reaya mwana wa Shobali akamzaa Yahathi, Yahathi akawazaa Ahumai na Lahadi. Hizo zilikuwa koo za Wasorathi. Hawa walikuwa wana wa Etamu: Yezreeli, Ishma na Idbashi. Dada yao aliitwa Haselelponi. Penueli akamzaa Gedori, naye Ezeri akamzaa Husha. Hawa walikuwa wazao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, na baba yake Bethlehemu. Ashuri baba yake Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara. Hawa walikuwa wazao wa Naara: Ahuzamu, Heferi, Temeni na Haahashtari. Wana wa Hela walikuwa: Serethi, Sohari, Ethnani, na Kosi ambaye aliwazaa Anubi, Sobeba na jamaa zote za Aharheli mwana wa Harumu.