1 Mambo ya Nyakati 4:1-8
1 Mambo ya Nyakati 4:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Wana wa Yuda walikuwa Peresi, Hesroni, Karmi, Huri na Shobali. Reaya, mwana wa Shobali, alimzaa Yahathi, aliyekuwa baba yake Ahumai na Lahadi, hizo ndizo jamaa za Wasorathi. Wana wa Etamu walikuwa Yezreeli, Ishma na Idbashi. Walikuwa na dada mmoja aliyeitwa Haselelponi. Penueli aliwazaa Gedori na Ezeri, na Ezeri akamzaa Husha. Hao ndio wazawa wa Huri mzaliwa wa kwanza wa Efratha, baba yake Bethlehemu. Ashuru, mwanzilishi wa mji wa Tekoa, alikuwa na wake wawili: Hela na Naara. Naara alimzalia wana wanne: Ahuzamu, Heferi, Temeni na Haahashtari. Hela alimzalia wana watatu: Serethi, Ishari na Ethnani. Hakosi aliwazaa Anubi na Sobeba, na ndiye aliyekuwa baba wa jamaa za wazawa wa Aharheli, mwana wa Harumu.
1 Mambo ya Nyakati 4:1-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wana wa Yuda; Peresi, na Hesroni, na Karmi, na Huri, na Shobali. Na Reaya, mwana wa Shobali, akamzaa Yahathi; na Yahathi akawazaa Ahumai, na Lahadi. Hizo ndizo jamaa za Wasorathi. Na hawa ndio wana wa babaye Etamu; Yezreeli, na Ishma, na Idbashi; na dada yao aliitwa jina lake Haselelponi; na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, babaye Bethlehemu. Naye Ashuri, babaye Tekoa, alikuwa na wake wawili, Hela na Naara. Naye Naara akamzalia Ahuzamu, na Heferi, na Temeni, na Ahashtari. Hao ndio wana wa Naara. Na wana wa Hela walikuwa Serethi, na Ishari, na Ethnani. Na Hakosi akawazaa Anubu, na Sobeba, na jamaa za Aharheli, mwana wa Harumu.
1 Mambo ya Nyakati 4:1-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wana wa Yuda; Peresi, na Hesroni, na Karmi, na Huri, na Shobali. Na Reaya, mwana wa Shobali, akamzaa Yahathi; na Yahathi akawazaa Ahumai, na Lahadi. Hizo ndizo jamaa za Wasorathi. Na hawa ndio wana wa babaye Etamu; Yezreeli, na Ishma, na Idbashi; na umbu lao aliitwa jina lake Haselelponi; na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, babaye Bethlehemu. Naye Ashuri, babaye Tekoa, alikuwa na wake wawili, Hela na Naara. Naye Naara akamzalia Ahuzamu, na Heferi, na Temeni, na Ahashtari. Hao ndio wana wa Naara. Na wana wa Hela walikuwa Serethi, na Ishari, na Ethnani. Na Hakosi akawazaa Anubu, na Sobeba, na jamaa za Aharheli, mwana wa Harumu.
1 Mambo ya Nyakati 4:1-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wazao wa Yuda walikuwa: Peresi, Hesroni, Karmi, Huri na Shobali. Reaya mwana wa Shobali akamzaa Yahathi, Yahathi akawazaa Ahumai na Lahadi. Hizo zilikuwa koo za Wasorathi. Hawa walikuwa wana wa Etamu: Yezreeli, Ishma na Idbashi. Dada yao aliitwa Haselelponi. Penueli akamzaa Gedori, naye Ezeri akamzaa Husha. Hawa walikuwa wazao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, na baba yake Bethlehemu. Ashuri baba yake Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara. Hawa walikuwa wazao wa Naara: Ahuzamu, Heferi, Temeni na Haahashtari. Wana wa Hela walikuwa: Serethi, Sohari, Ethnani, na Kosi ambaye aliwazaa Anubi, Sobeba na jamaa zote za Aharheli mwana wa Harumu.