Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 114:1-8

Zab 114:1-8 SUV

Haleluya. Israeli alipotoka Misri, Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni. Yuda ilikuwa patakatifu pake, Israeli milki yake. Bahari iliona ikakimbia, Yordani ilirudishwa nyuma. Milima iliruka kama kondoo waume, Vilima kama wana-kondoo. Ee bahari, una nini, ukimbie? Yordani, urudi nyuma? Enyi milima, mruke kama kondoo waume? Enyi vilima, kama wana-kondoo? Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana, Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo. Augeuza mwamba kuwa ziwa la maji, Jiwe gumu kuwa chemchemi.

Soma Zab 114

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 114:1-8

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha