Zab 105:12-15
Zab 105:12-15 SUV
Walipokuwa watu wawezao kuhesabiwa, Naam, watu wachache na wageni ndani yake, Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa, Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine. Hakumwacha mtu awaonee, Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao. Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.

