Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mit 3

3
Maonyo juu ya Kumwamini na Kumheshimu Mungu
1 # Kum 30:16 Mwanangu, usiisahau sheria yangu,
Bali moyo wako uzishike amri zangu.
2Maana zitakuongezea wingi wa siku.
Na miaka ya uzima, na amani.
3 # Kum 6:8; Yer 17:1; 2 Kor 3:3 Rehema na kweli zisifarakane nawe;
Zifunge shingoni mwako;
Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
4 # Lk 2:52; 1 Sam 2:26; Mdo 2:47 Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri,
Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.
5 # Yer 9:23 Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,
Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
6 # 1 Nya 28:9; Yer 10:23 Katika njia zako zote mkiri yeye,
Naye atayanyosha mapito yako.
7 # Rum 12:16 Usiwe mwenye hekima machoni pako;
Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.
8Itakuwa afya mwilini pako,#3:8 Au, kitovuni pako.
Na mafuta mifupani mwako.
9 # Kut 23:19 Mheshimu BWANA kwa mali yako,
Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
10 # Kum 28:8 Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi,
Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.
11 # Ayu 5:17; Ebr 12:5 Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na BWANA,
Wala usione ni taabu kurudiwa naye.
12 # Ufu 3:19; Kum 8:5 Kwa kuwa BWANA ampendaye humrudi,
Kama vile baba mwanawe ampendezaye.
Utajiri wa Kweli
13Heri mtu yule aonaye hekima,
Na mtu yule apataye ufahamu.
14 # Ayu 28:13; Mit 2:4; 8:11,19 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha,
Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.
15 # Mt 13:44 Yeye ana thamani kuliko marijani,
Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.
16 # 1 Tim 4:8 Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume,
Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.
17 # Mt 11:29 Njia zake ni njia za kupendeza sana,
Na mapito yake yote ni amani.
18 # Mwa 2:9 Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana;
Ana heri kila mtu ashikamanaye naye.
Hekima ya Mungu katika Uumbaji
19 # Mit 8:27; Yn 1:3; Ebr 1:2 Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya nchi;
Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;
20 # Kum 33:28; Ayu 36:28 Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika;
Na mawingu yadondoza umande.
Usalama wa Kweli
21Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako,
Shika hekima kamili na busara.
22Basi yatakuwa uzima kwa nafsi yako,
Na neema shingoni mwako.
23Ndipo utakapokwenda katika njia yako salama,
Wala mguu wako hautakwaa.
24 # Law 26:6 Ulalapo hutaona hofu;
Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu.
25Usiogope hofu ya ghafula,
Wala uharibifu wa waovu utakapofika.
26Kwa kuwa BWANA atakuwa tumaini lako,
Naye atakulinda mguu wako usinaswe.
27 # Rum 13:7; Gal 6:10 Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao,
Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.
28 # Law 19:13; Kum 24:15 Usimwambie jirani yako,
Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa;
Nawe unacho kitu kile karibu nawe.
29Usiwaze mabaya juu ya jirani yako,
Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama.
30 # Rum 12:18 Usishindane na mtu bila sababu,
Ikiwa hakukudhuru kwa lo lote.
31Usimhusudu mtu mwenye jeuri,
Wala usiichague mojawapo ya njia zake.
32Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa BWANA,
Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.
33 # Zek 5:4; Mal 2:2; Zab 1:3 Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu,
Bali huibariki maskani ya mwenye haki.
34 # Yak 4:6; 1 Pet 5:5; Zab 138:6; Mt 23:12 Hakika yake huwadharau wenye dharau,
Bali huwapa wanyenyekevu neema.
35 # Dan 12:2 Wenye hekima wataurithi utukufu,
Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha.

Iliyochaguliwa sasa

Mit 3: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha