Mit 3:5-9
Mit 3:5-9 SUV
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu. Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako. Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.