Methali 3:5-9
Methali 3:5-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtumaini Mwenyezi-Mungu kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe. Umtambue Mungu katika kila ufanyalo, naye atazinyosha njia zako. Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima; mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu. Hiyo itakuwa dawa mwilini mwako, na kiburudisho mifupani mwako. Mheshimu Mwenyezi-Mungu kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
Methali 3:5-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Usiwe na hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu. Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako. Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
Methali 3:5-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu. Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako. Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
Methali 3:5-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako. Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe; mche BWANA ukajiepushe na uovu. Hii itakuletea afya mwilini mwako, na lishe kwenye mifupa yako. Mheshimu BWANA kwa mali yako na kwa malimbuko ya mazao yako yote