Mit 29:5-8
Mit 29:5-8 SUV
Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake. Kuna mtego katika kosa la mtu mbaya; Bali mwenye haki huimba na kufurahi. Mwenye haki huyaangalia madai ya maskini; Bali mtu mbaya hana ufahamu hata ayajue. Watu wenye dharau huwasha mji moto; Bali wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu.