Mithali 29:5-8
Mithali 29:5-8 NENO
Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili, anautandaza wavu kuitega miguu yake. Mwovu hutegwa na dhambi yake mwenyewe, bali mwenye haki hushangilia na kufurahi. Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini, bali mwovu hajishughulishi na hilo. Wanaodhihaki huuchochea mji, bali wenye hekima huzuia hasira.