Methali 29:5-8
Methali 29:5-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenye kumbembeleza jirani yake, anatega mtego wa kujinasa mwenyewe. Mtu mbaya hunaswa kwa kosa lake, lakini mtu mwadilifu huimba na kufurahi. Mwadilifu anajua haki za maskini, lakini mtu mwovu hajui mambo hayo. Wenye dharau huutia vurugu mji mzima, lakini wenye hekima hutuliza ghadhabu.
Methali 29:5-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake. Kuna mtego katika kosa la mtu mbaya; Bali mwenye haki huimba na kufurahi. Mwenye haki huyaangalia madai ya maskini; Bali mtu mbaya hana ufahamu hata ayajue. Watu wenye dharau huwasha mji moto; Bali wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu.
Methali 29:5-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake. Kuna mtego katika kosa la mtu mbaya; Bali mwenye haki huimba na kufurahi. Mwenye haki huyaangalia madai ya maskini; Bali mtu mbaya hana ufahamu hata ayajue. Watu wenye dharau huwasha mji moto; Bali wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu.
Methali 29:5-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili, anautandaza wavu kuitega miguu yake. Mwovu hutegwa na dhambi yake mwenyewe, bali mwenye haki hushangilia na kufurahi. Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini, bali mwovu hajishughulishi na hilo. Wanaodhihaki huuchochea mji, bali wenye hekima huzuia hasira.