Mit 26:23-28
Mit 26:23-28 SUV
Midomo ijipendekezayo pamoja na moyo mbaya Ni kama kigae kilichofunikizwa taka za fedha. Achukiaye huficha chuki kwa midomo yake; Naye huweka akiba ya hila moyoni mwake. Anenapo maneno mazuri usimsadiki; Kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake. Ingawa chuki hufunikizwa kwa hila; Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko. Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia. Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi; Na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.