Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 26:23-28

Mithali 26:23-28 NENO

Kama rangi ingʼaayo iliyopakwa kwenye vyombo vya udongo ndivyo ilivyo midomo laini pamoja na moyo mbaya. Mtu mwenye nia ya kudhuru wengine hujificha kwa maneno ya midomo yake, lakini moyoni mwake huficha udanganyifu. Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini, kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake. Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu, lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko. Mtu akichimba shimo, atatumbukia ndani yake; mtu akivingirisha jiwe, litamrudia. Ulimi wa uongo huwachukia wale unaowaumiza, nacho kinywa cha kujipendekeza husababisha uharibifu.