Mit 24:15-18
Mit 24:15-18 SUV
Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika; Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya. Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo; BWANA asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake.