Zaburi 72:10-14
Zaburi 72:10-14 NENO
Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali watamletea ushuru; wafalme wa Sheba na Seba watampa zawadi. Wafalme wote watamsujudia na mataifa yote yatamtumikia. Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia, aliyeonewa asiye na wa kumsaidia. Atawahurumia wanyonge na wahitaji na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti. Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili, kwani damu yao ni ya thamani machoni pake.


