Mithali 28:1-6
Mithali 28:1-6 NENO
Mtu mwovu hukimbia ingawa hakuna yeyote anayemfukuza, bali wenye haki ni wajasiri kama simba. Nchi inapokuwa na uasi, inakuwa na viongozi wengi, bali kiongozi mwenye ufahamu na maarifa hudumisha utaratibu. Mtawala anayewadhulumu maskini, ni kama mvua ya dhoruba inayoharibu mazao yote. Wale wanaoacha sheria huwasifu waovu, bali wale wanaotii sheria huwapinga. Wapotovu hawaelewi haki, bali wale wanaomtafuta BWANA wanaielewa kikamilifu. Afadhali maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama, kuliko tajiri ambaye njia zake ni potovu.