Methali 28:1-6
Methali 28:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Waovu hukimbia japo hawafukuzwi na mtu, lakini waadilifu ni hodari kama simba. Taifa la fujo huzusha viongozi wengi, lakini kwa kiongozi mmoja mwenye akili na maarifa huwa na utengemano Mtu mhitaji anayewadhulumu maskini, amefanana na mvua kubwa inayoharibu mimea. Watu wanaovunja sheria huwasifu waovu, lakini wanaoishika sheria hupingana nao. Waovu hawajui maana ya haki, lakini wamchao Mwenyezi-Mungu wanaielewa kabisa. Afadhali maskini aishiye kwa unyofu, kuliko tajiri aishiye kwa upotovu.
Methali 28:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba. Kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi; Bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa Mtu mhitaji awaoneaye maskini, Ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza chakula. Wao waiachao sheria huwasifu waovu; Bali wao waishikao hushindana nao. Watu waovu hawaelewi na haki; Bali wamtafutao BWANA huelewa na zote. Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotovu wa njia angawa ni tajiri.
Methali 28:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba. Kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi; Bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa Mtu mhitaji awaoneaye maskini, Ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza chakula. Wao waiachao sheria huwasifu waovu; Bali wao waishikao hushindana nao. Watu wabaya hawaelewi na hukumu; Bali wamtafutao BWANA huelewa na yote. Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake, Kuliko mpotofu wa njia angawa ni tajiri.
Methali 28:1-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mtu mwovu hukimbia ingawa hakuna yeyote anayemfukuza, bali wenye haki ni wajasiri kama simba. Nchi inapokuwa na uasi, inakuwa na viongozi wengi, bali kiongozi mwenye ufahamu na maarifa hudumisha utaratibu. Mtawala anayewadhulumu maskini, ni kama mvua ya dhoruba inayoharibu mazao yote. Wale wanaoacha sheria huwasifu waovu, bali wale wanaotii sheria huwapinga. Wapotovu hawaelewi haki, bali wale wanaomtafuta BWANA wanaielewa kikamilifu. Afadhali maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama, kuliko tajiri ambaye njia zake ni potovu.