Mithali 26:24-26
Mithali 26:24-26 NENO
Mtu mwenye nia ya kudhuru wengine hujificha kwa maneno ya midomo yake, lakini moyoni mwake huficha udanganyifu. Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini, kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake. Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu, lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko.