Methali 26:24-26
Methali 26:24-26 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenye chuki huficha chuki yake kwa maneno mazuri, lakini huwa ana hila moyoni mwake. Akiongea vizuri usimwamini, moyoni mwake mna chuki chungu nzima. Huenda akaficha chuki yake, lakini nia zake mbaya zitajulikana kwa wote.
Methali 26:24-26 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Achukiaye huficha chuki kwa midomo yake; Naye huweka akiba ya hila moyoni mwake. Anenapo maneno mazuri usimsadiki; Kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake. Ingawa chuki hufunikwa na hila; Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko.
Methali 26:24-26 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Achukiaye huficha chuki kwa midomo yake; Naye huweka akiba ya hila moyoni mwake. Anenapo maneno mazuri usimsadiki; Kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake. Ingawa chuki hufunikizwa kwa hila; Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko.
Methali 26:24-26 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mtu mwenye nia ya kudhuru wengine hujificha kwa maneno ya midomo yake, lakini moyoni mwake huficha udanganyifu. Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini, kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake. Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu, lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko.