Mithali 20:5-14
Mithali 20:5-14 NENO
Makusudi ya moyo wa mwanadamu ni maji yenye kina, lakini mtu mwenye ufahamu huyachota. Watu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma, bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata? Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama, wamebarikiwa watoto wake baada yake. Mfalme anapoketi kwenye kiti chake cha ufalme kuhukumu, hupepeta ubaya wote kwa macho yake. Ni nani awezaye kusema, “Nimeuweka moyo wangu safi; mimi ni safi na sina dhambi?” Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti, BWANA huchukia vyote viwili. Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake, kama tabia yake ni safi na adili. Masikio yasikiayo na macho yaonayo: BWANA ndiye alivifanya vyote viwili. Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini, uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba. “Haifai, haifai!” asema mnunuzi, kisha huondoka akijisifia ununuzi wake.