Methali 20:5-14
Methali 20:5-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Fikira za mtu zimefichika kama kilindi cha maji; lakini mtu mwenye busara ajua kuzichota humo. Watu wengi hujivunia kuwa wema, lakini mwaminifu wa kweli apatikana wapi? Mtu mwadilifu akiishi kwa unyofu; watoto wake atakaowaacha watabarikiwa. Mfalme mwema aketipo kutoa hukumu, huupepeta uovu wote kwa macho yake. Nani athubutuye kusema: “Nimeutakasa moyo wangu; mimi nimetakasika dhambi yangu?” Mizani ya udanganyifu na vipimo vya udanganyifu, vyote ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu. Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake, kama tabia yake ni njema na aminifu. Sikio lisikialo na jicho lionalo, yote mawili kayafanya Mwenyezi-Mungu. Usipende kulala tu usije ukawa maskini; uwe macho nawe utakuwa na chakula kingi. “Hakifai, hakifai”, mnunuzi hulalamika, lakini akiondoka hujisifu amepunguziwa bei.
Methali 20:5-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mashauri ya moyoni ni kama kilindi; Lakini mtu mwenye ufahamu atayateka. Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe; Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata? Mwenye haki aendaye katika unyofu wake, Watoto wake wabarikiwa baada yake. Mfalme aketiye katika kiti cha hukumu, Huyapepeta mabaya yote kwa macho yake. Nani awezaye kusema, Nimesafisha moyo wangu; Nimetakasika dhambi yangu? Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali, Vyote viwili ni chukizo kwa BWANA. Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake; Kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili. Sikio lisikialo, na jicho lionalo, BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili. Usipende usingizi usije ukawa maskini; Fumbua macho yako nawe utashiba chakula. Haifai kitu, haifai kitu, asema mnunuzi; Lakini akiisha kwenda zake hujisifu.
Methali 20:5-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Methali 20:5-14 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Makusudi ya moyo wa mwanadamu ni maji yenye kina, lakini mtu mwenye ufahamu huyachota. Watu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma, bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata? Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama, wamebarikiwa watoto wake baada yake. Mfalme anapoketi kwenye kiti chake cha ufalme kuhukumu, hupepeta ubaya wote kwa macho yake. Ni nani awezaye kusema, “Nimeuweka moyo wangu safi; mimi ni safi na sina dhambi?” Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti, BWANA huchukia vyote viwili. Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake, kama tabia yake ni safi na adili. Masikio yasikiayo na macho yaonayo: BWANA ndiye alivifanya vyote viwili. Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini, uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba. “Haifai, haifai!” asema mnunuzi, kisha huondoka akijisifia ununuzi wake.