Kwa hiyo Mungu aliwatupa, waingiwe na tamaa za upujufu. Kwani hata wanawake wao wakayageuza matumikio yao ya kimtu, wakazusha mengine yasiyo ya kimtu. Vile vile hata waume wakaacha kuwatumia wanawake kimtu, tena kwa hivyo, tamaa zao zilivyowachoma kama moto, wakatumiana waume na waume wenzao; wakafanya hayo yasiyopasa kamwe, wakapata malipo ya upotevu wao yaliyowapasa. Tena kwa hivyo, walivyokataa kumshika Mungu na kumtambua, Mungu aliwatupa, wafuate mawazo ya ujinga na kufanya yasiyompasa mtu.