Kwenu ninyi visiwe hivyo ila mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu sharti awe mtumishi wenu! Naye anayetaka kuwa wa kwanza kwenu sharti awe mtumwa wenu! Kama Mwana wa mtu asivyokuja, atumikiwe, ila amekuja kutumika na kuitoa roho yake kuwa makombozi ya watu wengi.