1
Mateo 13:23
Swahili Roehl Bible 1937
SRB37
Lakini zilizomiagwa penye mchanga mzuri ni kama mtu anayelisikia Neno na kulijua maana. Ndiye mwenye kuzaa, mwingine huleta punje mia, mwingine sitini, mwingine thelathini.
Linganisha
Chunguza Mateo 13:23
2
Mateo 13:22
Lakini zilizomiagwa penye miiba ni kama mtu anayelisikia Neno, lakini masumbuko ya dunia hii na udanganyifu wa mali hulisonga Neno, lisizae matunda.
Chunguza Mateo 13:22
3
Mateo 13:19
Kila anayelisikia Neno la ufalme asipolijua maana, huja yule Mbaya na kulinyakua lililomiagwa moyoni mwake. Hizo ndizo zilizomiagwa njiani.
Chunguza Mateo 13:19
4
Mateo 13:20-21
Lakini zilizomiagwa penye miamba ni kama mtu anayelisikia Neno na kulipokea papo hapo kwa furaha. Lakini hana mizizi moyoni mwake, ila analishika kwa kitambo kidogo tu. Yanapotukia maumivu au mafukuzo kwa ajili ya Neno, mara hujikwaa.
Chunguza Mateo 13:20-21
5
Mateo 13:44
*Ufalme wa mbingu umefanana na fedha zilizofukiwa shambani. Mtu alipoziona akazifukia, akaenda kwa furaha yake, akaviuza vyote, alivyokuwa navyo, akalinunua shamba lile.
Chunguza Mateo 13:44
6
Mateo 13:8
Lakini nyingine zikaangukia penye mchanga mzuri, zikazaa, nyingine punje mia, nyingine sitini, nyingine thelathini.
Chunguza Mateo 13:8
7
Mateo 13:30
Acheni, zikue zote mbili pamoja, mpaka mavuno yatakapokuwa! Siku za kuvuna nitawaambia wavunaji: Kusanyeni kwanza nyasi, mzifunge matitatita, mziteketeze! Lakini ngano zitieni chanjani kwangu!*
Chunguza Mateo 13:30
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video