1
Kutoka 6:6
Neno: Bibilia Takatifu 2025
NENO
“Kwa hiyo, waambie Waisraeli: ‘Mimi ndimi BWANA, nami nitawatoa katika nira ya Wamisri. Nitawaweka huru mtoke kuwa watumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyooshwa pamoja na matendo makuu ya hukumu.
Linganisha
Chunguza Kutoka 6:6
2
Kutoka 6:7
Nitawachukua ninyi kuwa watu wangu mwenyewe, nami nitakuwa Mungu wenu. Ndipo mtajua kuwa mimi ndimi BWANA Mungu wenu, niliyewatoa chini ya nira ya Wamisri.
Chunguza Kutoka 6:7
3
Kutoka 6:8-9
Nami nitawaleta hadi nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kumpa Abrahamu, Isaka na Yakobo. Nitawapa iwe milki yenu. Mimi ndimi BWANA.’ ” Musa akawaarifu Waisraeli jambo hili, lakini hawakumsikiliza kwa sababu ya kuvunjika moyo na kazi yao ngumu.
Chunguza Kutoka 6:8-9
4
Kutoka 6:1
Kisha BWANA akamwambia Musa, “Sasa utaona kitu nitakachomfanyia Farao: Kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawaachia watu waende; kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawafukuza waondoke nchini mwake.”
Chunguza Kutoka 6:1
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video