Kutoka 6:8-9
Kutoka 6:8-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Nami nitawapeleka katika nchi ile niliyoapa kumpa Abrahamu, Isaka na Yakobo. Nitawapeni nchi hiyo iwe yenu. Mimi ni Mwenyezi-Mungu.’” Mose akawaeleza Waisraeli maneno hayo. Lakini wao hawakumsikiliza kwa sababu walikuwa wamekufa moyo kutokana na utumwa mkali.
Kutoka 6:8-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo niliinua mkono wangu, niwape Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA. Musa akawaambia wana wa Israeli maneno haya; lakini hawakumsikiliza Musa kwa ajili ya uchungu wa moyo, na kwa ajili ya utumwa mgumu.
Kutoka 6:8-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo naliinua mkono wangu, niwape Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA. Musa akawaambia wana wa Israeli maneno haya; lakini hawakumsikiliza Musa kwa ajili ya uchungu wa moyo, na kwa ajili ya utumwa mgumu.
Kutoka 6:8-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nami nitawaleta hadi nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kumpa Abrahamu, Isaka na Yakobo. Nitawapa iwe milki yenu. Mimi ndimi BWANA.’ ” Musa akawaarifu Waisraeli jambo hili, lakini hawakumsikiliza kwa sababu ya kuvunjika moyo na kazi yao ngumu.