YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 02/2024Sample

Soma Biblia Kila Siku 02/2024

DAY 28 OF 29

Mungu anaweka mwongozo wa namna ya kutoa, kuandaa na kisha kutekeleza kafara. Upo wajibu kwa watoao, na pia upo wajibu wa kikuhani. Mungu anapenda utaratibu, ubora na utakatifu visitenganishwe. Kumwabudu Mungu kuheshimiwe. Kwa sababu ya utaratibu wake, Mungu anaita watumishi kwa mpango maalumu. Watumishi wake anawaweka wakfu na kuwabariki hadharani. Watumishi wa Mungu wa kweli kamwe hawajiiti na kujiweka wakfu wenyewe. Mungu anaita na kutambulisha wateule wake kwa jamii inayotumikiwa.

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 02/2024

Soma Biblia Kila Siku 02/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu

More